Staa wa Muziki wa Bongofleva Harmonize ameendelea kutupasha mapya kuhusiana na ujio wa album yake mpya ambayo ameipa jina la HIGH SCHOOL.
Akiwa kwenye moja ya interview wiki hii, Harmonize amesema album hiyo tayari imekamilika kila kitu, anachosubiri ni kuona ratiba za wasanii wenzake kwenye label na kisha ataidondosha.
Kingine kikubwa ambacho Konde Boy amekifanya kwenye album yake hii ya Pili ni kutoshirikisha wasanii wa nje ya Tanzania, kama alivyofanya kwenye ‘Afro East’ ambayo ilisheheni majina mazito ya Afrika na dunia.
Harmonize amesema anataka kuwakaribisha watu kwenye Darasa lake na kuwaonesha sisi kama Wana Afrika Mashariki tunaweza kufanya aina yoyote ya muziki.