Sauti ya mwimbaji kutoka marekani T-Pain kwenye nyimbo zake ilikuwa tofauti na wasanii wengine kutokana na sauti yake kuwa ya kipekee, ambayo kitaalam inaitwa (auto-tune) ambayo ni effect maalum inayotumika kwenye studio za muziki.
Japo msanii huyo alipitia ukosoaji mkubwa kutoka kwa wasanii wengi nchini marekani akiwemo Jay-Z lakini hakukata tamaa kwenye shughuli zake za kimuziki.
Sasa mkali huyo wa ngoma”Bartender” ameibuka na kujinasibu kwamba wasanii wengi wa kisasa wanatumia auto-tune kuzinogesha nyimbo zao na yeye ndiye amewashawishi.
Kwenye mahojiano na Black Girl Nerds, T-Pain amesema kitendo cha wasanii kukumbatia auto tune inaonyesha ni jinsi gani walikuwa inspired na ubunifu wake.
“Kwa namna ilivyosambaa na namna ambavyo kila mmoja anaitumia kwa sasa, hiyo inanifanya nitambue kwamba nilikuwa nafanya kitu sahihi tangu awali. Kwa sababu kama ningekuwa sifanyi kitu sahihi, hakuna yeyote ambaye angefanya kwa sasa. Kwanini U-Copy kitu ambacho ni kibaya?” amesema T-Pain.