Rapa kutoka nchini Nigeria Lil frosh ataendelea kukaa gerezani hadi mwezi Machi kutokana na madai ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake ” Gift Camille” mwisho wa mwaka 2020.
Shtaka liliwasilishwa dhidi ya rapa huyo katika korti ya hakimu wa jimbo la Lagos huko Yaba ikisaidiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Wanasheria Wanawake, tawi la Jimbo la Lagos.
Katika kusikilizwa kwa kesi hiyo Jumanne,wiki hii mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Machi 9, mwaka wa 2021.,
Kulingana na ripoti, Lil Frosh atabaki mahabusu chini ya gereza hadi siku inayofuata iliyotajwa ya kusikilizwa kwa kesi yake.Mwaka 2020 mwishoni kulikuwa na taarifa za rapa Lil Frosh kumpiga aliyekuwa mpenzi wake ” Gift Camille” .
Kufuatia madai hayo dhidi ya Lil Frosh, lebo yake ya zamani DMW inayoongozwa na davido ilisitisha mkataba wake licha ya rapa huyo kukataa mara kadhaa tuhuma hizo za kumshambulia mpenzi wake.