Staa wa muziki nchini Sudi Boy ametangaza ujio wa album yake mpya ambayo ana mpango wa kuiachia hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Sudi Boy ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ya Mombasani ameweka ujumbe unaoashiria ujio wa album yake mpya umekamilika ambapo amewataka mashabiki zake wakae mkao wakula kwa ajili ya album hiyo.
Hata hivyo hajeweka wazi idadi ya ngoma wala jina la album yake mpya ila itakuwa ni album yake ya tatu baada ya Amini Mimi na Kaba.