Msanii wa Bongo Fleva, Baba Levo amekanusha kuwa kauli yake haikumlenga Mwanamitindo na msanii Hamisa Mobetto kama inavyotafsiriwa na baadhi ya watu mtandaoni na Hamisa mwenyewe.
Baba Levo alipangua madai hayo na malalamiko yaliyotafsiriwa kumlenga Hamisa kupitia video yake ambayo ilianza kusambazwa mitandaoni anayosikika akisema ‘Misa’ anaweza kujifungua ‘Mbwa’.
Baada ya kusambaa kwa video hiyo, Hamisa kupitia Insta Story kwenye mtandao wa Instagram alishusha lawama za moja kwa moja kwa msanii huyo akionesha kutopendezwa na kauli hiyo ya Baba Levo.
Hata hivyo muda mchache baada ya lawama za Hamisa, Baba Levo kupitia akaunti yake ya Instagram alikanusha madai hayo na na kueleza kuwa hajamtaja Hamisa kama inavyotafsiriwa bali alisema ‘Misa’.