Watu wawili wamekamatwa na Polisi nchini Uganda kwa kosa la kuchapa viboko Sanamu yenye sura ya Rais Yoweri Museveni.
Luta Ferdinand Male na Nsereko Asharf, ambao wanajiita wanaharakati waliipiga viboko sanamu kwa kuishutumu kufanya udanganyifu katika Uchaguzi Mkuu wa Uganda.
Uchaguzi wa Mkuu wa Uganda ulifanyika Januari 14 ambapo Rais Museveni alitangazwa kuwa mshindi na mshindani wake akilaumu kuwa kumekuwa na udanganyifu