DENMARK YASITISHA KWA MUDA UTOAJI WA CHANJO YA COVID-19

You are currently viewing DENMARK YASITISHA KWA MUDA UTOAJI WA CHANJO YA COVID-19

Denmark imesitisha utoaji wa Chanjo ya Oxford-AstraZeneca kwa muda wa wiki mbili ili kuchunguza ripoti za baadhi ya Wagonjwa kupata tatizo la Damu kuganda siku chache baada ya kuchanjwa.

Waziri wa Afya amesema wamechukua hatua hiyo ikiwa sehemu ya tahadhari ili kuchunguza endapo kuna madhara zaidi yaliyojitokeza tofauti na la Damu kuganda.

Mamlaka ya Afya ya Denmark imesema uamuzi wa kusimamisha Chanjo umekuja baada ya Mwanamke wa miaka 60 Nchini humo kupewa dozi ya AstraZeneca na kupoteza maisha.

Mpaka sasa Nchi 6 Duniani zimesitisha matumizi ya Chanjo ya AstraZeneca kutokana na madhara mbalimbali. Nchi hizo ni Austria, Estonia, Lithuania, Luxembourg, Latvia na Denmark.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa