Nyota wa muziki wa Bongofleva, msanii TID ametangaza ujio wa ziara yake ya kimuziki inayoitwa ‘Nyota 21’.
Akizungumza na waandishi wa habari, tid amesema, ameipa ziara hiyo jina la Nyota 21 kwa sababu ametimiza miaka hiyo tangu aanze kufanya kazi hiyo.
Baadhi ya wasanii ambao watakuwepo kwenye ziara hiyo ni G Nako, Lulu Diva, Linah, Domo Kaya na Sholo Mwamba.
Dodoma ndiyo litakuwa Jiji la kwanza kuanzisha burudani ya ziara hiyo huku Miji mingine kama Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam zikifuata.