Rapa kutoka nchini Marekani roddy ricch ametangaza ujio wa album yake ya “Feed Tha Street 3” japo hajaweka wazi tarehe rasmi ya kuiachia album hiyo.
Kupitia Instastory yake kwenye mtandao wa Instagram rapa roddy ricch amepost picha ya mkono wenye tattoo iliyoandikwa “Feed Tha Street” na kuandika 3, hivyo watu wametafsiri moja kwa moja kuwa rapa huyo yupo njiani kuiachia album hiyo sehemu ya 3.
Feed Tha Street ya kwanza ilitoka November 22, mwaka wa 2017 ikiwa na jumla ya nyimbo 17 huku Feed Tha Street ya pili ikitoka November 2, mwaka wa 2018 ikiwa na jumla ya nyimbo 12.
Tuendelee kusubiri taarifa zaidi kutoka kwa rapa roddy ricch kuwa ni lini ataiachia Feed Tha Street ya 3 na itakuwa na jumla ya nyimbo ngapi.