Chapa ya mavazi ya mwanamuziki kutoka nchini Marekani Rihanna iitwayo “Savage and Fenty” imetajwa kufikisha thamani ya shillingi billlioni 109 za Kenya.
Rihanna mwenye utajiri wa shillingi billioni 65.7 alizindua chapa hiyo ya mavazi mwaka 2018, ni miongoni mwa biashara za Rihanna ikiwemo Fenty Clothing Line, Fenty Beauty kwa ajili ya makeup na Fenty Skin kwa ajili ya vipodozi vya ngozi.
Ongezeko la thamani ya chapa hiyo limetokana na Series B funding, mradi ambao hufanywa kuchangisha fedha kutoka kwa wawekezaji na wafanya biashara kuchangia biashara zinazokua.
Hivyo baada ya mchakato huo, Savage X Fenty iliongeza pato lake hadi kufikia kiasi cha shillingi billioni 12.6 na kuifanya chapa hiyo kuwa na thamani ya shillingi billioni 109.