Mataifa yanayositisha kutoa chanjo ya COVID-19 ya AstraZeneca ili kujiridhisha kuhusu usalama wa chanjo yaongezeka baada ya Thailand kutangaza kusitisha matumizi ya chajo hiyo.
Mshauri wa Kamati ya Taifa ya Kusamimia Chanjo ya Virusi vya Corona wa Thailand amesema hawana sababu ya kuwa na haraka katika utoaji chanjo hivyo wanalenga kujiridhisha kuhusu usalama wa chanjo.
Mataifa mengine yaliyositisha chanjo ni Denmark, Norway, Iceland, Italia na Romania ambayo yalitangaza hatua hiyo jana
AstraZeneca imekuwa ikiwekewa wasiwasi kuwa inasababisha Damu Kuganda lakini baadhi ya Mamlaka za Afya Duniani zinasisitiza kwamba chanjo hiyo ni salama