Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Spice Diana amefunguka kwa mara ya kwanza tangu wafuasi wa Bob Wine watishia kususia muziki wake.
Hitmaker huyo wa ngoma ya Kokonya anaamini kuwa wapinzani wake wanafadhili watesi wake kwenye mitandao ya kijamii kuzima juhudi zake za kuupeleka muziki wake kwenye level nyingine.
Akipiga stori na radio moja nchini uganda spice diana amesema kuna ubinafsi mwingi miongoni mwa wasani nchini uganda na wengi wamekuwa wakimpiga vita kuhakikisha anafeli kwenye muziki wake lakini amehapa kupambana nao kwa kutoa muziki mzuri.
Ikumbukwe mapema wiki iliyopita wafuasi wa bob wine walitishia kususia muziki wa Spice Diana baada ya msanii huyo kukaa kimya kuhusu ishu ya Bob Wine kufungiwa nyumbani kwake mara baada ya matokeo ya uchaguzi nchini Uganda kutangazwa.