Nyota wa muziki wa Bongofleva Vanessa Mdee amezitaja filamu 3 alizoshiriki mpenzi wake Rotimi ambaye ni msanii wa filamu na muziki kutoka nchini Marekani zinazotarajiwa kuachiwa hivi karibuni.
Filamu alizozitaja ni pamoja na ‘Coming 2 America’ moja kati ya filamu zinazosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa filamu duniani, zingine ni ‘For the Love of Money’ na ‘Favorite Son’
Vanessa Mdee, amemsifia mpenzi akidai kuwa sio mzembe bali ni mchapakazi na mwenye kujituma katika kufanya kazi.
Rotimi alimvisha pete ya uchumba mwanadada Vanessa Mdee mwishoni mwa mwezi disemba mwaka wa 2020, kinachosubiriwa kwa sasa kwa wapenzi hao ni ndoa tu.