Maprodyuza Timbaland na Swizz Beatz kutoka marekani wameripotiwa kuiuza VERZUZ kwa kampuni ya Triller Network ambao ni wamiliki wa mtandao wa Triller.
VERZUZ ni jukwaa la muziki mtandaoni ambalo lilianzishwa na Timbaland pamoja na Swizz Beatz March mwaka wa, 2020.
Jukwaa (platform) hilo liliwapa nafasi wasanii kutunishiana misuli kwa kazi zao kushindanishwa, Verzuz ilijizolea umaarufu mkubwa hasa kipindi cha janga la COVID-19.
Dau la Triller kuinunua Verzuz halijawekwa wazi lakini imearifiwa kwamba Timbaland na Swizz beatz wamekuwa wanahisa wakubwa wa Triller Network na pia watakuwa miongoni mwa wahusika kwenye bodi ya Triller & Verzuz wakiwa na jukumu la kutengeneza mawazo na ubunifu.
Pia wamegawana sehemu ya mauzo na wasanii wote 43 ambao walishiriki kutumbuiza kwenye Verzuz tangu ianzishwe hadi leo hii.