Mwanamuziki kutoka nchini Uganda John Blaq amefunguka na kusema kwamba hana mpango wa kuoa hivi karibuni.
Akiwa kwenye moja ya interview hitmaker huyo wa ngoma ‘Dont Be Like’ amesema mapenzi yake kwenye muziki ndio yamemfanya haishi maisha mazuri licha ya changamoto anazokutana nazo.
John Blaq Anaamini wanawake wanaweza kumuaharibia shughuli zake za muziki lakini pia kumfilisisha kiuchumi.
Kauli ya John Blaq inakuja mara baada ya kuulizwa kuhusu maisha yake ya mahusiano.