OCTOPIZZO AMTOLEA UVIVU ITUMBI BAADA YA KUWAITA VIJANA WA KIBRA WAHUNI.

You are currently viewing OCTOPIZZO AMTOLEA UVIVU ITUMBI BAADA YA KUWAITA VIJANA WA KIBRA WAHUNI.
  • Post category:Burudani

Mkali wa rap nchini Octopizzo amewataka wanasiasa na viongozi wengine kukoma kuwatumia Vijana wa Kibra kwa masilahi yao ya kibinafsi na faida zao za kisiasa.

Kauli ya Octo imekuja mara baada ya Dennis Itumbi kudai kwamba vijana wa kibra walikodishwa kwenda kuchoma mikokoteni na wheelbarrow huko Githurai, wakati wa ziara ya Raila Odinga katika eneo hilo jumatato wiki hii.

Akijibu kuhusu suala hilo, Octopizzo amemwonya Itumbi kukoma kueneza propaganda kwa kusema kuwa vijana wa Kibra ni wakora.

Hata hivyo hitmaker huyo wa ngoma ya Goodmorning Africa amesema kuwa wanasiasa wanapaswa kujiepusha na ishu ya kuwatumia vijana wa Kibra kama wahuni kwani kitendo hicho kinaendelea kuharibu sifa zao.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa