SANAIPEI:NISIPOOLEWA NITABEBA MSALABA WANGU SIO WA JAMII.

You are currently viewing SANAIPEI:NISIPOOLEWA NITABEBA MSALABA WANGU SIO WA JAMII.
  • Post category:Burudani

Msanii wa kike nchini Sanaipei Tande amedai kuwa ataolewa muda sahihi ukifika na asipoolewa huo ni mzigo wake mwenyewe na wala sio wa jamii.

Akipiga stori na runinga moja nchini Sanaipei  mwenye umri wa miaka 35 amesema kwa sasa hana mpango wa kufunga ndoa licha ya kubezwa na watu, hivyo ameelekeza nguvu zake zote kwenye suala la kuupeleka muziki wake kwenye level nyingine.

Mkali huyo wa ngoma ya Nyota ameyasema hayo mara baada ya kuulizwa ni lini ataingia kwenye ndoa swali ambalo limekuwa likiulizwa na wadau wengi wa muziki nchini.

Ikumbukwe Sanaipei Tande alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Andrew Manga ambaye ni binamu wa Marehemu E-Sir kwa takriban miaka kumi lakini walikuja wakaachana miaka sita iliyopita baada ya uhusiano wao kukumbwa na dosari

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa