Wizara ya Afya inafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba maslahi ya wahudumu wa afya yanashughulikiwa ili kuimarisha sekta ya afya.
Akizungumza baada ya kuongoza shughuli ya kuchanjwa kwa wahudumu wa afya katika hospitali ya Rufaa ya Kenyatta Katibu katika Wizara ya Afya Dakta Susan Mochache amesema ni wajibu wa serikali kuhakikisha kwamba maafisa wa afya wanashughulikiwa ipasavyo.
Mochache amesema wizara ya afya imeweka mikakati kabambe kuhakikisha kwamba shughuli ya kuwapa chanjo wakenya inafwata utartibu unaofaa.
Naye katibu katika wizara ya afya dakta Patrick Amoth ambaye amekuwa afisa wa umma wa kwanza kupokea chanjo hiyo amewataka wahudumu wa afya na wakenya kwa ujumla kutokuwa na hofu ya chanjo hiyo akisema imefanyiwa utafiti wa haiba ya juu hivyo ni salama.