SERIKALI YA KAUNTI Y TURKANA IMEHAPA KUKABILI JANGA LA NZIGE WA JANGWANI.

Serikali ya kaunti ya Turkana imeahidi kuweka mikakati zaidi kukabiliana na tatizo la nzige wa jangwani ambalo linaendelea kushuhudiwa katika baadhi ya maeneo kaunti hiyo.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari gavana wa kaunti ya Turkana Josphat Nanok amesema serikali yake tayari imewatuma maafisa wa nyanjani  katika maeneo atharika ili kunyunyizia dawa katika maeneo ambayo yameathirka zaidi.

Aidha Nanok amesema serikali kaunti ya turkana kwa ushirikiano  na Shirika la Chakula Duniani FAO zinaendeleza juhudi za kuhakikisha wadudu hao wanaangamizwa kabisa katika maeneo yanayozalisha chakula kaunti hiyo kuzuia uwezekano wa kuwepo na upungufu wa chakula

Wakati huo huo amewataka washirika wengine wa maendeleo kuungana na serikali ya kitaifa,kaunti na Shirika la Chakula Duniani FAO katika mapambano dhidi ya nzige wa jangwani kaunti hiyo.

Hata hivyo ametoa wito kwa wakaazi wa kaunti ya turkana kutoa taarifa muhimu kwa mamlaka husika endapo watashuhudiwa visa vya uvamizi wa nzige wa jangwani katika maeneo yao ili kuwasaidia maafisa wa nyanjani kukabili na wadudu hao.

Robert Elim

Presenter and News Editor at North Rift Radio Kenya