Wito umetolewa kwa wanasiasa kukumbatia siasa za sera na maendeleo badala ya kujihusisha na siasa za kuwagawanya wakenya.
Akihutubu katika eneo bunge la Chearangani, Mshauri Mkuu wa Kisheria katika Afisi ya Naibu wa Rais Dkt Adrahama Singoei. ambaye amatangaza kuwania kiti cha ugavana Kaunti ya TransNzoia amewashauri wenyeji kaunti hiyo kuwa siasa za maneno matupu imepitwa na wakati , hivyo ni wajibu wa wananchi kuwapiga msasa wale wote wanaotafuta uongozi nchini kwa kufuata utendakazi wao.
Aidha Dkt Singoei ametoa wito kwa umma kujiepusha na siasa za migawanyiko na badala yake kukumbatia umoja wa kitafa kwa kuwachagua viongozi watakaowatekelezea maendeleo na kuwajibikia vyema matumizi ya fedha za umma kwa ajili ya maendeleo Kaunti hiyo.