WANANCHI WASHAURIWA KURIPOTI VISA VYA UKEKETAJI JIMBO LA POKOT MAGHARIBI.

You are currently viewing WANANCHI WASHAURIWA KURIPOTI VISA VYA UKEKETAJI JIMBO LA POKOT MAGHARIBI.

Ili kukabiliana vilivyo na visa vya ukeketaji katika Kaunti ya Pokot Magharibi ipo haja ya wananchi kuripoti visa hivyo katika Idara husika ili hatua madhubuti zichukuliwe. 

Akizungumza na meza yetu ya habari Mkurugenzi mkuu wa Shirika la vijana la Declares Group Kenya Mudaki Jefferson anasema watu wengi wana uoga wa kuripoti visa vya ukeketaji akisema hali hiyo inalemaza juhudi za kukabiliana na ukeketaji.

Aidha Mudaki amesema kuripotiwa kwa visa vingi vya ukeketaji maeneo ya mashinani mwaka jana kulichangiwa pakubwa na ujio wa virusi vya corona nchini.

Kampeni ya kuhamamisha jamii dhidi ya ukeketaji Pokot Magharibi pamoja na kuafikia hitaji la Serikali la kumaliza ukeketaji ifikapo mwaka 2022 inaanza tarehe 2 mwezi huu wa Februari ambapo mashariki ya Dws, Declaires Group Kenya, World Vision na Serikali miongoni mwa mashirika mengine ndio walengwa katika kampeni hiyo ambayo itazinduliwa na Kaunti Kamishna Pokot Magharibi Apollo Okello.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.