SERIKALI IMETAKIWA KUWEKA MIKAKATI MIPYA KUHUSU SHUGHULI YA UCHIMBAJI MAFUTA TURKANA KWA MANUFAA YA WANANCHI

  • Post category:County News

Serikali imetakiwa kujipanga ili uchimbaji wa rasilimali ya mafuta katika kaunti ya Turkana usisababishe kupanda kwa gharama za maisha na kuharibu uchumi wa nchi.

Mkurungezi mkuu wa Shirika la Marafiki wa Turkana Akal Ang’elei ametoa tahadhari hiyo akisema kuwa nchi nyingi duniani ambazo zimegundua kuwepo kwa nishati hiyo zimengia kwenye matatizo ya kiuchumi badala ya mapato yake kutumika kwa ustawi wa jamii.

Aidha Ange’lei amesema licha wakaazi wa kaunti ya turkana kuwa na matarajio mengi kuhusu manufaa yatakayoletwa na shughuli ya uchimbaji wa mafuta katika eneo la lokichar wengi wamesali kwenye lindi  la umaskini kutokana na kukosa kufaidi moja kwa moja na mradi huo.

Hata hivyo ni vyema serikali ijiandae sasa kuhusu namna ya kutumia mapato ya mafuta  kwa ustawi wa wananchi wake kwani suala hilo lisipoangaliwa kwa kina huenda wakaazi wa kaunti ya Turkana wakakosa kufaidi na raslimali ya mafuta na madini.

Robert Elim

Presenter and News Editor at North Rift Radio Kenya