UWANJA WA NDEGE WA LODWAR YAPOKEA GARI LA ZIMA MOTO KUTOKA KWA SERIKALI KUU

  • Post Category:County News

Uwanja mdogo wa ndege ulioko eneo la Lodwar kaunti ya Turkana kwa mara ya kwanza umepokea gari la zima moto kutoka kwa serikali kuu kusaidia kukabili mikasa ya moto kaunti hiyo.

Akizungumza baada ya kupokea gari hilo Msimamizi wa uwanja huo Richard Monyocho amesema ni afueni kwa wakaazi wa kaunti yaTurkana kwani kumekuwa na mikasa mingi ya moto ambayo imepelekea watu wengi kukadiria hasara bila usaidizi wowote.

Aidha Monyocho amesema gari hilo la zima moto litatumika hususan katika uwanja wa ndege na iwapo mikasa ya moto itatokea nje ya uwanja huo watatoa msaada.

Wakati huo huo ametoa wito kwa wizara husika kuhakikisha kuna maji ya kutosha huku akiiomba serikali ya kaunti hiyo pia kuongeza gari lingine ikizingatiwa kuwa kaunti ya Turkana ina maeneo mengi.

Hata hivyo amesema kwa sasa kaunti ya Turkana ina maafisa wa kutosha wenye tajriba kuhusu mikasa ya moto huku wengine zaidi wakitarajiwa kuajiriwa punde tu janga la corona litakapo kamilika.

Robert Elim

Presenter and News Editor at North Rift Radio Kenya