WAZAZI MT. ELGON WAHIMIZWA KURUDISHA WATOTO SHULE.

Wito umetolewa kwa wazazi kutoka kaunti ndogo ya Cheptais eneo bunge la Mlima Elgon kuhakikisha  wanawarejesha wanao shuleni ili kuendelea na masomo yao kama njia moja itakayowawezesha kujikimu siku za usoni.

Akihutubu baada ya kuzuru vyama vya ushirika mbalimbali katika wadi ya Chesikaki Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Cheptais Samwel Towet, anasema ni lazima wanafunzi wote warejelee masomo yao huku akiwasihi kushirikiana  kwa karibu na vyombo vya usalama ili kukabili uwezekano wa utovu wa usalama.

Aidha Towet amewashauri wakaazi kutilia maanani kilimo cha kahawa akisema kitawawezesha kujikimu kimaisha.

Hata hivyo amepongeza baadhi ya vyama vya ushirika eneo hilo kwa kuanzisha miradi mbalimbali ambayo anasema itawafaidi pakubwa wakulima.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa