Mamlaka Nchini Senegal imeyaamuru mashirika yanayotoa huduma ya Intaneti (Internet) kuzima huduma hiyo Nchi nzima, huku maandamano ya kupinga kuzuiliwa kwa Kiongozi wa Upinzani yanazidi kuongezeka
Kulingana na NetBlocks, huduma ya intaneti kwa mitandao ya kijamii na programu za ujumbe, ikiwemo Facebook, WhatsApp na YouTube imezimwa mapema jana.
Ndani ya siku mbili zilizopita, angalau mtu mmoja aliuawa katika makabiliano kati ya Polisi na wafuasi wa Mwanasiasa wa Upinzani, Ousmane Sonko ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ubakaji na inadaiwa kukamatwa kwake kulichochewa kisiasa