Staa wa muziki wa dancehall duniani Sean Paul ametengua kauli yake ambayo aliitoa mwezi uliopita kwamba Jay-Z alimuonea wivu kipindi amefanya kolabo na Beyonce “Baby Boy” mwaka 2003.
Stori hiyo ilisema Jay-Z aliuua wimbo huo kwa sababu alikuwa akimkataza Sean Paul kukaa karibu na Beyonce na hata kufanya show pamoja.
Sasa kwenye mahojiano na HotNewHipHop, Sean Paul amesema hakusema hivyo, bali mtangazaji wa kituo kile cha redio, ndiye aliikuza na hadi kufika kwenye mitandao.