MEGAN THEE STALLION AJIBU TAARIFA ZA TORY LANEZ KUFUTIWA MASHTAKA

You are currently viewing MEGAN THEE STALLION AJIBU TAARIFA ZA TORY LANEZ KUFUTIWA MASHTAKA
  • Post category:Burudani

Rapa kike kutoka Marekani Megan Thee Stallion ameibuka na kunyoosha maelezo kuhusu taarifa za kufutwa kwa shtaka la Tory Lanez.

Kupitia twitter, Megan Thee Stallion amekuja na kusema watu wazipuuze habari hizo kwani shtaka liko pale pale. Tarehe ya kwanza ya kusikilizwa kwa kesi hiyo ilisogezwa mbele kutokana sherehe za kuapishwa kwa Rais.

Hata hivyo Megan ameapa lazima Tory Lanez afungwe. 

Baada ya mwaka 2020 kumalizika vibaya kwa upande wa rapa kutoka nchini Cannada Tory Lanez kwa kesi iliyokuwa inamsumbua kuhusu rapa wa kike Megan Thee Stallion basi amejipanga kuendelea na mwaka 2021 bila matatizo na mtu yeyote ila kikubwa anachokitazama kwa mwaka huu ni kuwapa kazi nzuri mashabiki zake.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Tory Lanez ameandika “Nitaendelea na mwaka 2021 bila matatizo,nataka kufanya maudhui kubwa kwa ajili ya mashabiki zangu,ninawapenda wote”.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa