Msaniii wa muziki nchini KRG the Don amemtolea uvivu msanii mwenzake Benzema aliyekuwa anaunda kundi la Ochungulo family ambalo lilivunjika majuzi.
Kupitia ukurasa wake wa instagram mkali huyo wa ngoma ya “Giddem” amempongeza wasanii Nelly the Goon na DMore kwa hatua ya kujitenga na Benzema ambaye alikuwa member wa kundi hilo akisema kuwa msanii huyo sio mtu mzuri ikija kwenye masuala ya biashara kwani ni tapeli.
Kauli hiyo ya Krg the Don haikupokelewa vyema na wadau wa muziki nchini ambao wamemchana msanii huyo akome kutumia lugha ya matusi kwa wasanii wengine ikizingatiwa kuwa hana idhibati ya kuonyesha Benzema ni tapeli.
Ikumbukwe KRG The Don hana uhusiano mzuri na Benzema tangu alipoibua madai kwamba Benzema alivuja pesa za miraba au royalties ya wimbo wao uitwao “Doremi” mwaka wa 2020.