HART THE BAND,SAUTI SOL & NYASHINSKI WATAJWA KWENYE ORODHA YA WASANII 100 BORA AFRIKA

You are currently viewing HART THE BAND,SAUTI SOL & NYASHINSKI WATAJWA KWENYE ORODHA YA WASANII 100 BORA AFRIKA
  • Post category:Burudani

Kituo cha Televisheni cha Burudani kutoka nchini Ghana “WatsUp TV” kimetangaza orodha ya Wanamuziki 100 wa Kiafrika walio Juu zaidi kwa mwaka wa 2021.

Orodha hiyo imewajumuisha wasanii kutoka Kenya kama Hart the Band,Sauti sol,Khaligraph Jones na Nyashinski ambao inadaiwa wanazidi kufanya vizuri kwenye muziki barani Afrika. 

Nchi ya Tanzania ina wasanii kama diamond platinumz,Ali kiba, harmonize, Rayvanny na Navy Kenzo huku Uganda ikiwa na Wasanii Eddy Kenzo, Bebe Cool, na Rema Namakula.

Orodha hiyo imekamilishwa na wanamuziki kutoka nchi 26 za Afrika ikiwa ni pamoja na Angelique Kidjo, Burna Boy, Davido, Wizkid, Cassper Nyovest, Sarkodie na wasanii wengine.

Orodha hiyo ina jumla ya wasanii 18 wa kike na wasanii 73 wa kiume huku makundi yakiwa 9,katika orodha hiyo msanii mdogo zaidi ni msanii kutoka nchini Nigeria rema akiwa na miaka “20” na msanii mkubwa zaidi ni msanii kutoka Misri Mohammed mouniro akiwa na miaka “66”. 

Nigeria imeongoza kwa kutoa wasanii 26 katika orodha hiyo wakifuatiwa na Ghana wasanii 10,Ivory Coast 7 na Afrika kusini wasanii 6.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa