Kolabo ya Beyonce na Sean Paul “Baby Boy” ya mwaka 2003 ilikuwa miongoni mwa ngoma kali na zilizotamba sana, huenda ingekuwa kubwa zaidi kama sio wivu wa Jay-Z.
Sean Paul amefunguka kupitia mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini Jamaica ambapo amesema baada ya Kolabo hiyo, Jay-Z hakutaka kabisa mkali huyo wa dancehall awe karibu na mkewe Beyonce.
Mtangazaji alianza kwa kusema kwamba hakufurahishwa na namna collabo hiyo ilivyofanyika, Sean Paul alipigilia msumari kwa kusema
“Sikuweza kujisikia ‘comfortable’ lakini Mimi nilitumia tu hekima na busara pale unapokutana na vikwazo kwenye maisha.” alisema Sean Paul na kukazia kwamba Jay-Z alikuwa na wivu na ndio maana walionekana mara chache sana wakitumbuiza pamoja wimbo huo Jukwaani.