Msanii Mkongwe wa muziki Wyclef Jean mzaliwa wa Haiti aliyehamia Marekani amehamua kushare post ya kipande cha video ya wimbo wa ‘GoodVibes’ wake, Lady Jaydee.
Jean ambaye jina lake kamili ni Nel Ust Wyclef Jean, alishare post ya video ya wimbo huo wa Lady Jaydee unapatikana kwenye album ya ’20’ kupitia Insta Story yake kwenye mtandao wa Instagram.
Lady Jaydee kwa furaha kupitia akaunti yake ya Instagram alipost ujumbe wa shukrani kwa Wyclef Jean na kueleza kuwa hatua ya mkongwe huyo ni yenye maana kubwa sana kwake.