Rapa kutoka nchini Marekani Kodak Black amekuwa mtu mwema sana tangu awe uraiani mara baada ya kupokea msamaha wa Donald Trump.
Sasa ametangaza nia ya kuwalipia ada watoto wa maafisa wawili wa FBI ambao waliuawa wakiwa kazini wiki iliyopita mjini Florida.
Tovuti ya TMZ imeripoti kwamba Kodak Black pamoja na mwanasheria wake Bradford Cohen wamepeleka barua kwenye kitengo cha FBI mjini Miami na kuomba kuruhusiwa kutoa msaada huo wa kwa watoto wa maofisa hao, Daniel Alfin na Laura Schwartzen berger.