Staa wa muziki nchini Magix Enga amewatolea uvivu baadhi ya watu wanaotumia jina lake kuwatapeli wasanii wanaotaka kurekodi nae muziki kwenye rekodi lebo ya Magix Empire.
Kupitia insta story yake ya kwenye ukurasa wake Instagram Magix Enga ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki nchini amekanusha taarifa za kuwa tapeli wasanii na kusema kwamba hajawahi kufanya biashara yeyote akitumia namba tofauti za simu.
Kutokana na hilo magix enga amewaonya wanaotapeli wasanii wanaotaka kufanya nae kazi kukoma mara moja la sivyo watakutana na mkono wa sheria huku akiwataka mashabiki zake kuwa makini na matapeli hao wanaotumia jina lake kujipatia pesa.