RANDY ORTON AKASIRISHWA NA KAULI YA SOULJA BOY KWAMBA MICHEZO YA MIELEKA NI MAIGIZO

You are currently viewing RANDY ORTON AKASIRISHWA NA KAULI YA SOULJA BOY KWAMBA MICHEZO YA MIELEKA NI MAIGIZO
  • Post category:Burudani

Kauli ya Rapa Soulja Boy kutoka nchini Marekani kwamba mchezo wa Mieleka hauna uhalisia (fake) umemkasirisha mwanamieleka wa WWE, Randy Orton. 

Wawili hao wamejibizana vikali kwenye mtandao wa twitter huku Randy akionesha wazi hasira zake.

Kubwa lililomkera Randy Orton ni Soulja Boy kuudhihaki mchezo ambao unamfanya apate kipato na aishi vizuri na familia yake.

Soulja Boy anaonekana kama amejipanga kwani alienda mbali zaidi hadi kutaka kuzichapa na Randy kama yupo tayari. 

Staa mwingine alionekana kukerwa na kauli hiyo ya  mkali huyo.wa ngoma ya ‘The Crank That’, ni T-BAR wa kundi la Retribution.

Hii imekuja kufuatia mapema wiki hii, Soulja Boy kuandika kupitia ukurasa wake wa twitter kwamba game ya Hip Hop kwa sasa imekuwa feki kama ulivyo mchezo wa mieleka chini ya WWE.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa