Rapa Quavo ametupasha habari njema kuhusu ujio wa album ya kundi la Migos iitwayo “Culture 3” ambayo imesubiriwa kwa muda sasa na mashabiki wa kundi hilo.
Juzi kati Quavo akiwa anapata chakula cha usiku na mpenzi wake Saweetie, Paparazzi walimfuata na kumuuliza swali kuhusu album hiyo, kwa haraka haraka alijibu kwamba itatoka hivi karibuni,kwani imebaki takribani mwezi mmoja na nusu.
Culture 3′ itakuwa album ya Nne ya kundi la Migos baada ya Culture 2 iliyotoka mwezi Januari , mwaka wa 2019