Msanii wa kike nchini Uganda Evelyn Lagu amelazwa hosptilani kwa miaka mitatu sasa kutokana na matatizo ya figo.
Juzi kati alitangaza anahitaji kupandikiziwa figo ili aweze kuishi kwa muda mrefu na matibabu yake yatagharimu shillingi millioni 7.5.
Kutokana na hilo, hafla ya kuchangisha pesa ilifanyika wikiendi hii iliyopita jijini kampala ambapo shillingi laki 6 ilikusanywa kwa ajili ya kugharamia matibabu ya msanii huyo.
Sasa baadhi ya Mashabiki wa muziki nchini uganda wamewataka wasanii Jose Chameleone, Bebe Cool na Bob Wine wachangishe fedha za kugharamia matibabu ya msanii Evelyn lagu.
Hii ni baada ya wasanii hao kukosa kufika au kutuma wawakilishi wao kwenye hafla ya kuchangisha fedha za kugharamia matibabu ya evelyn lagu iliyofanyika Jiji Kampala licha ya wanamuziki hao kuwa matajiri.