DADDY OWEN ATOA NENO KWA WANAOPITIA MSONGO WA MAWAZO MAISHANI.

You are currently viewing DADDY OWEN ATOA NENO KWA WANAOPITIA MSONGO WA MAWAZO MAISHANI.
  • Post category:Burudani

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Daddy Owen amekuwa akipatia mambo mengi kwenye maisha yake mara baada ya kuachana na mke wake Faridah Wambui.

Moja kati ya mambo ambayo amekuwa akipambana nao kwenye maisha yake ni msongo wa mawazo tangu ndoa yake ilipoingiwa na dosari mwaka wa 2019.

Kutokana na hilo Daddy Owen kwa sasa yupo kwenye hatua za kurejea katika hali ya kawaida kutokana na ushauri ambao anazidi kuupata kutoka kwa mshauri wake wa afya ya akili.

Sasa mkali huyo wa ngoma ya “Vanity” kupitia ukurasa wake wa Instagram amewahimiza watu ambao wanapitia changamoto ya msongo wa mawazo maishani kujitokeza na kuzungumzia hali zao ili waweze kupata usaidizi wa haraka kwani wakichukulie poa suala hilo huenda wakaathirika kiakili.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa