Staa wa muziki nchini Uganda Ykee Benda ametangaza ujio wa album yake ya pili baada ya miezi kadhaa ya kurekodi nyimbo zitakazopatikana kwenye album hiyo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ykee Benda ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa “RadioMan” amesema album hiyo ameipa jina la “Kirabo” na ana mpango wa kuitoa mwaka huu wa 2021.
Hata hivyo hajeweka wazi idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye album hiyo ila amewataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kwani “Kirabo” itakuwa imebeba ladhaa tofauti sana ambayo wamekuwa wakiikosa kwa muda mrefu.
Iwapo Ykee Benda atafanikiwa kuiachia album ya “Kirabo” itakuwa ni album yake ya pili baada ya “Kireka Boy” iliyotoka mwaka wa 2017.