Staa wa muziki nchini Kevin Bahati amefunguka kuhusu suala la watu kumuita mtoto wa Diana.
Kupitia ukurusa wake wa Instagram mkali huyo wa ngoma ya ‘Tomato” amesema haoni shida yeyote watu wakimuita mtoto wa diana kwani mke wake huyo anamuonyesha mapenzi aliyokosa kutoka kwa mamake mzazi ambaye alitangulia mbele za haki.
Haikuishia hapo bahati alienda mbali zaidi na kuweka wazi kwamba kipindi wanachumbiana na mkewe diana marua aliwahi kumuueleza kwamba anatamani kumuona akimuonyesha mapenzi kama ya mamake mzazi.
Hata hivyo baada ya kuona ujumbe huo mkewe Diana Marua alijibu kwa kusema kuwa hawezi kumpa msanii huyo mapenzi kama ya mamake mzazi bali atampa mapenzi kama mkewe.