Chama cha Kitaifa cha wazazi katika kaunti ya Trans nzoia kimeelezea kuridhishwa na agizo la wizara ya elimu kwa watahiniwa wa darasa la nane kuchagua upya shule za upili watakazojiunga nazo kwenye kaunti ndogo.
Mwenyekiti wa chama hicho Wellington Waliaula anasema hatua hiyo itatoa fursa mwafaka kwa wazazi kufuatilia mienendo ya wanao na kuwapa mawaidha nasaha kukabili mikasa ya moto shuleni.
Waliaula amesema wazazi wamekuwa wakigharamika mno kwa kuchanga fedha za kujenga upya majengo yaliyoteketezwa shuleni na kutoa wito kwa serikali kufanya uchunguzi wa kina ikiwamo wasimamizi wa shule kubainisha chanzo cha visa hivyo.
kadhalika ameirai Wizara ya Elimu kuingilia kati na kuwachukulia hatua kali za kisheria wakuu wa shule wanaowatuma watahiniwa wa darasa la nane na kidato cha nne nyumbani wakati ambapo wanatarajiwa kufanya mitihani ya kitaifa kcpe na KCSE mwezi ujao.