Bosi wa lebo ya muziki ya Gagamel msanii Bebe Cool anajulikana sana kwa kumshambulia Bob Wine kila mara kwenye masuala mengi yanayohusu nchini Uganda.
Na mara nyingi kitu chochote kikitokea mashabiki wengi wa muziki nchini Uganda huwa na matarajio makubwa kuwa Bebe Cool hawezi kumzaza Bob Wine lakini inaonekana mambo yamebadilika.
Kwenye moja ya interview bebe cool amedinda kuzungumzia sakata la gari la kifahari lilomkabili Bob Wine.
Bebe Cool ambaye wiki iliyopita alidai anamiliki gari la kuzuia risasi kama la Bob Wine, amesema haoni kitu cha maana cha kuzungumzia kuhusiana na sakata la Bob Wine.
Kutokana hilo ametoa wito kwa mashabiki wa muziki nchini Uganda kuangazia mambo ya maendeleo kuliko kuzungumzia sakala la Bob Wine ambalo halina tija kwa jamii..