Viongozi wa kidini katika kaunti ya Bungoma wamesikitishwa na visa vya wanafunzi katika kaunti hiyo kugoma na kusababisha uharibifu mkubwa katika shule mbalimbali na kutaka walimu wakuu kupitia wizara ya elimu kuwaruhusu wahubiri katika shule hizo ili waweze kutoa ushauri nasaha kwa wanafunzi .
Wakizungumza na wanahabri mjini Webuye viongozi hao wa kidini wakiongozwa na mwenyekiti wa ushirika wa Webuye Alex Masika pamoja na Esther Ngijabe wamesema kuwa wanafunzi wengi wanakumbwa na msongo wa mawazo baada ya kukaa nyumbani kwa muda mrefu kutokana na janga la Korona na ingekuwa vyema kwao kupata ushauri wa kila mara wakiendelea na masomo yao.
Hata hivyo viongozi hao wa kidini wametoa hisia mseto kuhusiana na kurejeshwa kwa adhabu ya viboko shuleni huku wengine wakisema adhabu hiyo ilipitwa na wakati huku wengine wakisema kuwa viboko vinapaswa kurejeshwa shuleni.