Msanii wa muziki wa Rap nchini Tanzania, Bill Nass amefuta picha na video zote kwenye ukurasa wake wa Instagram, hatua iliyohisiwa kuwa ni maandalizi ya kuachia kazi mpya hivi karibuni.
Hatua hii ya Bill Nass imevuta hisia za baadhi ya mashabiki ikihisiwa kuwa huenda akaachia wimbo mpya baada ya kufanya vizuri na wimbo wa ‘Do Me’ alioshirikishwa na Nandy.
Uamuzi wa Bill Nass hakujali hata picha alizopiga na Mpenzi wake, Nandy huku upande mwingine ikihisiwa kuwa pengine kuna kingine kisichohusiana na ujio wa kazi kutoka kwake.