Staa wa muziki nchini Esther Akoth maarufu kama Akothee amesema kuwa anaogopa kupata Uja Uzito kuliko virusi vya Covid-19 kwa sababu tu wanaume wa siku hizi hawatoi matunzo kwa watoto wao.
Kauli hiyo inakuja mara baada ya kuwadanganya wafuasi wake na uchunguzi bandia wa ujauzito,huku akisisitiza kuwa yeye ni mjamzito.
Aidha ametoa wito kwa mashabiki wake wamruhusu aendelee kuota ndoto ya kupata ujauzito, bila ya kuifanya iwe kweli.
Mwanamuziki huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo wake uitwao Dende Yom amekuwa akizungumzia suala la kupata mtoto kwa muda sasa ambapo mwezi Agosti mwaka jana, alikuwa na tamaa ya kupata mtoto wa sita.