Msanii nguli wa HipHop duniani Snoop Dogg anasema aliacha ku-rap kuhusu vifo kufuatia kufariki kwa Tupac Shakur na Notorious BIG.
Kwenye mahojiano na Fatman Scoop, Snoop Dogg aliongelea mabadiliko hayo kwenye utunzi wake kufuatia vifo vya manguli hao wa Hip Hop duniani lakini pia mambo ambayo yaliwahi kumtokea kutokana na maudhui ya nyimbo zake.
Alitukumbusha kwamba aliwahi kuandika ‘Murder Was the Case’ wimbo ambao baadaye ulikuja kumtokea kwa kupata kesi ya mauaji mwaka 1993.
Akitolea mifano ya nyimbo kama ‘Death Around the Corner’ na ‘If I Die Tonight’ za Tupac Shakur na ‘Life After Death’ album ya Biggie, na baadaye vifo vyao vilifuatana kwa wote kupigwa risasi.