Tutaanza kumuona rapa Quavo kutoka nchini Marekani kwenye filamu za Hollywood, ametajwa kushiriki filamu yake ya kwanza akiwa na waigizaji Robert DeNiro, John Malkovich, na Jack Huston.
Filamu hiyo iitwayo “Wash Me in the River” kwa sasa inaandaliwa nchini Puerto Rico.
Kwa mujibu wa mtandao wa Variety, Quavo atacheza uhusika wa muuza madawa za kulevya mashuhuri ambaye anaitwa Coyote kwenye filamu hiyo ya mapigano.
“Kiukweli nafikiri hii filamu itaenda kuwa moja kati ya filamu kubwa kuwahi kutoka kipindi hichi.” alisema Quavo