Waandaaji wa Tuzo kubwa za muziki Duniani Grammy wametangaza list ya wasanii watakaotumbuiza katika hafla ya utoaji Tuzo za 63 za Grammy mwaka wa 2021.
Rapa Cardi B, Megan Thee Stallion na Lil Baby wametajwa kudondosha Burudani wakati wa hafla hiyo inayotarajiwa kufanyika Machi 14, mwaka 2021 huko Los Angeles, nchini Marekani.
Roddy Ricch ,Post Malone, Doja Cat, DaBaby, na Taylor Swift pia watatumbuiza wakati wa sherehe hiyo, ambayo itazingatia miongozo ya usalama wa COVID-19.
Wasanii wengine ni pamoja na Dua Lipa, BTS, Harry styles, Bad Bunny na Chris Martin.
Katika Tuzo za Grammy 2021 Beyoncé ndiye ameteuliwa katika Vipengele 9 akifuatiwa na Taylor Swift, Dua Lipa, na Roddy Ricch wakiwa na Vipengele sita kila mmoja.
Host wa Sherehe ya Tuzo hizo za kila mwaka atakuwa Trevor Noah kutoka Afrika kusini na, itaruka Mubashara kwenye runinga ya CBS Machi 14, mwaka huu baada ya kuahirishwa Januari 31 kutokana na kuongezeka kwa visa vya COVID-19 huko Los Angeles.