Staa wa muziki nchini Uganda Sheebah ametajwa kwenye orodha ya wasanii walioteuliwa kuwani tuzo za Nickelodeon Kids Choice mwaka wa 2021 kupitia kipengele cha Favourite African Star.
Sheebah ameshare taarifa hiyo nzuri kwa mashabiki zake kupitia mitandao yake kijamii huku akiwataka waanze kumpigia kura kupitia mtandao wa Twitter na tovuti rasmi ya KidsChoiceAwards.com
Sheebah ni msanii wa pili kutoka nchini uganda kutajwa kuwania tuzo hiyo baada ya kikundi cha watoto cha Triplets Ghetto kids.
Ikumbukwe mwaka wa 2020 wasanii Eddy Kenzo na Ann Kansiime walikuwa miongoni mwa wasanii kutoka uganda waliotajwa kuwania tuzo hizo.
Tuzo hizo za watoto za kampuni ya Nickelodeon zinatarajiwa kutolewa tarehe 15 Machi mwaka huu wa 2021.