Mashabiki wa msanii wa nyimbo za Injili nchini, Moji Short Baba, wametaka kuwa na uhakika ikiwa ni kweli mkali huyo amefunga ndoa.
Hiyo ni baada ya posti mpya kutoka kwa mkali huyo wa ngoma ya Imani kwenye ukurasa wake wa Instagram, ikimuonyesha akimvisha pete mpenzi wake wa siku nyingi Nyawira Gachugi wakiwa kwenye hafla ya siri iliyohudhuriwa na wanafamilia pamoja na marafiki.
Hata hivyo, kwenye posti hiyo Moji Short Baba amepokea pongezi nyingi kutoka kwa Mastaa wenzake, huku swali la ni lini amefunga ndoa likibaki bila majibu.