Naibu wa rais William Ruto amesema tatizo kubwa linalolikumba taifa hili si kufanyia marakebisho katiba kupitia mswada wa BBI ila ni kusuluhisha matatizo yanayokikumba mkenya wa kawaida kumwezesha kujiimarisha kiuchumi.
Akihutubu kwenye eneo bunge la Endebess Ruto amesema mpango kama ule wa ajenda kuu nne ya serikali ndio utakaostawisha taifa hili
Aidha Ruto amewarai washindani wake kusitisha siasa za ukabila na badala yake kuangazia sera za maendeleo kwa faida ya wananchi.
Kwa upande wake mwakilishi wa kike wa kaunti ya Trans-Nzoia, Janet Nangabo amemtaka rais uhuru kenyatta kuwaadhibu mawaziri wanaoendeleza siasa za mirengo badala ya kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa katiba.